NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko ya muundo wa Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji na Wizara ya Nishati kwa Wizara hizo kuwa na Makatibu Wakuu wawili kila moja, hatua inayolenga kuimarisha ufanisi wa utendaji na uhakika wa uongozi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Februari 6,2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi wa viongozi umefanyika kama ifuatavyo:
Wakuu wa Mikoa
Kanali Yahya Ramadhani Kido ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera akichukua nafasi ya Bi. Fatma Mwassa.
Kanali Donald William Msengi ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, akichukua nafasi ya Kanali Patrick Kenan Sawala ambaye atapangiwa majukumu mengine.
Makatibu Wakuu
Dkt. Tausi Mbaga Kida ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango.
Dkt.Fred Matola Msemwa ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Uwekezaji.
Balozi Waziri Rajab Salum ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara, akichukua nafasi ya Dkt.Hashil Twaib Abdallah ambaye atapangiwa majukumu mengine.

