NA SIXMUND BAGASHE
WIZARA ya Maliasili na Utalii inaendelea kutumia mbinu na teknolojia mbalimbali za kupambana na Wanyamapori wakali na waharibifu sambamba na kufungua fursa za uhifadhi na Utalii kupitia sekta za Maliasili na Utalii, kwa Watanzania ikiwemo Wilaya ya Mkinga iliyoko Mkoa wa Tanga.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameyasema hayo kwenye Mkutano wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameki Nchemba (Mb) na Wananchi wa Mkinga katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika Chuo Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Tanga.Dkt. Kijaji amesema kuwa, ni dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye Mhifadhi namba moja nchini, kuhakikisha wananchi wananufaika na uhifadhi wakiwa salama na wenye furaha.
"Vituo vya Askari wa kuzuia Wanyamapori wakali na waharibifu (PAC) vitajengwa katika eneo la vijiji vya Mwanyumba na Mavovo Wilayani Mkinga kwa sababu ndio eneo lenye changamoto kubwa ya tembo kwani ni mapito ya tembo kuelekea misitu ya mtoni bombo," amesema Dkt.Kijaji.
Akizungumza kwa niaba ya wanamkinga, Mbunge wa Jimbo la Mkinga Mhe.Twaha Mwakihoja (Mb) ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kazi kubwa ya uhifadhi na mapambano dhidi ya Wanyamapori wakali na waharibifu, nakuomba juhudi hizo ziongezeke zaidi sambamba na kufungua fursa zaidi ya kiuchumi kwa wananchi kupitia swkta ya Utalii.






