MARA-Wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya wilayani Bunda, wamesema wako tayari kushirikiana na TAKUKURU kudhibiti mianya ya rushwa katika utoaji wa huduma za afya pindi wanapotumia mifumo ya kielektroniki ya utoaji huduma hizo.
Mhe.Aswege Enock Kaminyoge, Mkuu wa Wilaya ya Bunda ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika warsha hiyo.
Ahadi hiyo imetolewa katika warsha iliyoandaliwa na TAKUKURU iliyohusu Udhibiti wa Mianya ya Rushwa katika Mifumo ya Utoaji Huduma za Afya inayotumiwa na Hospitali Teule ya Wilaya ya Bunda.
Dkt.Omari Ramadhan Mzee ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi-Udhibiti Rushwa kutoka TAKUKURU, akitoa salamu za Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo Wilayani Bunda.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau wa Sekta ya Afya na TAKUKURU, Mhe.Aswege Enock Kaminyoge, Mkuu wa Wilaya ya Bunda ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika warsha hiyo, amewahimiza wadau hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU wakati wote kwa manufaa ya jamii inayopata huduma.
Bw. Mohamed Shariff,Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mara akitoa shukrani kwa wadau wa Afya kwa ushirikiano wanaouonesha katika Mapambano Dhidi ya Rushwa wilayani Bunda na Mkoa wa Mara kwa ujumla.Pia, amewataka inapobidi waombe msaada wa kufanyiwa uchambuzi wa mifumo ya utendaji kazi ili kubaini mianya ya rushwa iliyopo na kuchukua hatua stahiki mapema.
Aidha, aliipongeza TAKUKURU na Menejimenti ya Hospitali Teule ya Wilaya ya Bunda kwa kuwa kielelezo tosha cha ushirikiano wa sekta binafsi na Serikali katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.
Warsha hii imefanyika Februari 19,2026 katika ukumbi wa Balili Rock Resort uliopo Bunda, ambapo majadiliano yaliongozwa na Bw. Marko Machele,Katibu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) Dayosisi mkoani Mara.
Dkt. Omari Ramadhan Mzee Mkurugenzi Msaidizi-Udhibiti Rushwa TAKUKURU akisalimiana na Bw. Salum Mtelela Katibu Tawala Wilaya ya Bunda, mara baada ya kuwasili kwenye Warsha ya Wadau wa Sekta ya Afya wilayani Bunda.
Akiongoza mjadala huo,Bw.Machelle alisema, vituo vya kutolea huduma za afya vinalenga kutoa huduma bora kwa wananchi na ili huduma hizo ziwe bora ni lazima kudhibiti vitendo vya rushwa itakayowezesha kupata mapato ya kutosha.

