DAR-Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, leo Februari 17, 2026 imekutana na Rais mstaafu wa Jumuiya ya Wanasheria Tanzania (Tanganyika Law Society-TLS), Dkt.Edward Hosea.

Mkutano huo wa Tume na Dkt.Hosea umefanyika katika ukumbi wa Tanganyika uliopo jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mkoani hapa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Tume kukusanya taarifa, maoni na ushauri kutoka kwa viongozi mbalimbali.
Katika mkutano huo hoja zilizojadiliwa zilihusu maeneo ya tathmini ya athari za matukio hayo ndani ya nchi na kimataifa na ushauri wa hatua za kijamii na kisheria zinazochukuliwa ili kuimarisha amani, mshikamano wa kitaifa.
Tume inaendelea kukutana na makundi mbalimbali ikiwemo waathirika wa matukio ya uvunjifu wa amani, kwa lengo la kukusanya ushahidi na taarifa zitakazoiwezesha kuandaa ripoti ya kina.


