Tume,Mufti wateta matukio ya Oktoba 29

DAR-Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, leo Februari 27, 2026 imekutana na Kiongozi mkuu wa Masuala ya Sheria ya Kiislamu na Uongozi wa Waislamu nchini Tanzania, Mufti Sheikh Abubakar Zubeir.
Mkutano huo wa Tume na Mufti umefanyika katika Ukumbi wa Lake Tanganyika uliopo jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jijini hapa.

Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni pamoja na namna matukio hayo yalivyoanza, athari zake kwa watu, mali na miundombinu pia ushauri wa namna ya kuondokana na matukio hayo.
Hivi karibuni Mamlaka ya Uteuzi imeiongezea Tume muda wa siku arobaini na mbili (42) kuanzia tarehe 20 Februari, 2026 ili Tume iweze kukamilisha uchunguzi wa matukio hayo ambapo imetakiwa ikamilishe kazi na kuwasilisha Taarifa yake kabla au ifikapo tarehe 3 Aprili, 2026.

Kwa sasa Tume inaendelea na mahojiano na watu mbalimbali wakiwemo waathirika wa matukio hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here