Tutatangaza tarehe ya kuanza mfungo-BAKWATA

DAR-Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) linatarajiwa kutangaza rasmi tarehe ya kuanza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kulingana na kuandama kwa mwezi. 
Aidha,taarifa rasmi hutolewa na Mufti wa Tanzania mara baada ya mwezi kuonekana ambapo mfungo unatarajiwa kuanza Februari 19,2026 au Februari 20,2026 kulingana na mwandamo wa mwezi.

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA Makao Makuu, Sheikh Hamisi Mataka amesema hayo Februari 17,2026 wakati akitoa taarifa kwa niaba ya BAKWATA jijini Dar es Salaam.

"BAKWATA inawakumbusha kuwa mwezi wa mwandamo wa Ramadhani tunautarajia Februari 18 itakuwa ndio mwezi 29 Shaban, ukiandamana tarehe 19 tutaingia katika mwezi mtukufu wa Ramadhan, usipoandama tutakamilisha tarehe 19 ambayo ni mwezi 30 na Ramadhan itaanza Februari 20...InshaAllah.

"Kubwa ambalo tunalisisitiza subirini taarifa kutoka BAKWATA lenyewe lina kamati maalum ya kufuatilia mambo ya mwezi kwa kushirikiana na nchi za Afrika Mashariki, Zanzibar na Kenya kule tunashirikiana nao wote na tunapothibitisha taarifa Mheshimiwa Mufti anatoa idhini na taarifa hizo wanatangaziwa Waislamu."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here