NA DIRAMAKINI
KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania (Twiga Stars),Bakari Shime ametangaza rasmi orodha ya wachezaji 30 walioteuliwa kushiriki kama kikosi cha awali katika maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026.
Kikosi hiki kinawakilisha mchanganyiko wa wachezaji wenye uzoefu pamoja na vipaji vipya wanaotarajiwa kutoa mchango mkubwa katika mashindano yatakayofanyika mwaka ujao.
Aidha, Kocha huyo amechagua wachezaji kutoka vilabu mbalimbali ndani na nje ya nchi, akizingatia ubora wa kiufundi, uwezo wa kimapambano na michakato ya maandalizi ya kimkakati kwa ajili ya mashindano ya kimataifa.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na TFF, kikosi hicho kina wachezaji wanaocheza katika klabu za ndani kama JKT Queens, Yanga Princess, Simba Queens, pamoja na nje ya nchi katika vilabu vya Juárez (Mexico), MFA Žalgiris (Lithuania), FC Masar (Misri), SD Eibar (Hispania), Al Nassr FC (Saudia), Brighton & Hove Albion (Uingereza) na Trabzonspor (Uturuki).
Orodha kamili ya wachezaji walioteuliwa ni kama ifuatavyo:
1. Najiath Abbas (JKT Queens)
2. Asha Mrisho (Mashujaa Queens)
3. Nusrat Jafar (Fountain Gate)
4. Husna Mtunda (Alliance Girls)
5. Enekia Kasonga (Juárez, Mexico)
6. Lidya Maximilian (JKT Queens)
7. Diana MnaIy (Yanga Princess)
8. Asha Omary (Simba Queens)
9. Donisia Minja (JKT Queens)
10. Juletha Singano (Juárez, Mexico)
11. Noela Luhala (MFA Žalgiris, Lithuania)
12. Christer Bahera (JKT Queens)
13. Anastazia Katunzi (JKT Queens)
14. Vaileth Nicholaus (FC Masar, Egypt)
15. Ester Maseke (JKT Queens)
16. Janeth Christopher (JKT Queens)
17. Suzan Adam (Tausi FC)
18. Maimuna Kaimu (Yanga Princess)
19. Joyce Lema (JKT Queens)
20. Elizabeth Chenge (JKT Queens)
21. Stumai Abdallah (JKT Queens)
22. Winfrida Gerald (JKT Queens)
23. Aisha Juma (Simba Queens)
24. Hasnath Ubamba (FC Masar, Egypt)
25. Opah Clement (SD Eibar, Spain)
26. Neema Shau (Yanga Princess)
27. Jamila Rajabu (JKT Queens)
28. Clara Luvanga (Al Nassr FC, Saudi Arabia)
29. Aisha Masaka (Brighton & Hove Albion, England)
30. Diana Lucas (Trabzonspor, Turkey).
