Waambieni wazazi wenu ukweli,msiwaogope

ARUSHA-Imeelezwa kuwa, ili kutokomeza ukatili wa kijinsia hususani kwa watoto ni vyema watoto wenyewe wakawa na utamaduni wa kuwaambia ukweli Wazazi au Walezi wao juu ya madhira mbalimbali ya ukatili wanaofanyiwa katika jamii.
Hayo yameelezwa leo na Mkaguzi Kata ya Oldonyosambu, Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Hamis Malegea wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi St. Peters Anglican kuhusu mradi wa Jeshi la Polisi wa POLISI NA WATOTO ambapo amewataka watoto hao kutowaogopa wazazi au walezi wao badala yake wawaambie ukweli kuhusu madhira na dalili za vitendo vya ukatili.

Aidha, Mkaguzi huyo, amesema kuwa katika vituo vya Polisi Nchini kumewekwa mazingira rafiki ya kuripoti taarifa mbalimbali za uhalifu ikiwa ni pamoja na ukatili dhidi ya Watoto hivyo ni vyema jamii pamoja na watoto wenyewe wakatumia fursa hiyo katika kushirikiana na Jeshi la Polisi kutokomeza ukatili katika Jamii.
Mradi wa Polisi na Watoto ulioanzishwa na Jeshi la Polisi Nchini kupitia Kamisheni ya Polisi jamii unalengo la kuwajengea uwezo Watoto kutambua changamoto mbalimbali za kiusalama zinazoweza kuwakabili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here