Wananchi kunufaika na AFCON kupitia Utalii

NA SIXMUND BAGASHE

WIZARA ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na wadau wa Utalii, inaendelea kujiandaa vyema katika kuhakikisha wageni watakao ingia nchini kwa ajili ya Michezo ya AFCON 2027, wanapata fursa adhimu ya kutembelea vivutio vya utalii hususani vilivyopo katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Akijibu hoja mbalimbali za wanachi Wilaya ya Moshi, walizo toa katika Mkutano wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Mwigulu Lameki Nchemba (Mb) na wananchi wa Moshi, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amesema kuwa maandalizi hayo nipamoja na kuboresha zaidi miundombinu na upatikanaji wa fursa zaidi za uwekezaji katika sekta hiyo.
Kuhusu mazao mapya ya utalii, Dkt. Kijaji amebainisha kuwa, juhudi kubwa iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya uhifadhi na Utalii inayopelekea wageni wengi kuja kutalii nchini, Wizara hiyo imejipanga vyema kuhakikisha mazao mapya ya utalii yanaongezeka ili kuunga mkono juhudi hiyo.
Licha ya kuwapongeza kwa kazi nzuri ya ushiriki wao katika Uhifadhi endelevu wa Maliasili nchini, amewashauri wananchi hao wa Moshi na Tanzania kwa ujumla kuendelea kuchangamkia fursa mbalimbali silizopo katika sekta ya uhifadhi na Utalii husani ajira

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here