Waziri wa Fedha ahitimisha ziara yake TRA

DAR-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amehitimisha ziara yake ya siku mbili katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jijini Dar es Salaam.
Februari 26,2026 alitembelea Idara ya Forodha, Kitengo cha Ufuatiliaji wa Usafirishaji (Transit Monitoring), Idara ya Upelelezi wa Kodi, Idara ya Kodi za Ndani na Timu ya inayosimamia Mfumo Mpya Jumuishi wa Kodi za Ndani (IDRAS).
Mheshimiwa Balozi Omar ameielekeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuimarisha usimamizi wa mizigo inayoingia nchini kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nchi jirani (transit), ili kudhibiti vitendo vya ukwepaji kodi vinavyofanywa na baadhi ya wadau wa forodha wasio waaminifu.
Ametoa maelekezo hayo jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara katika Idara ya Forodha kukagua namna ukusanyaji wa mapato unavyosimamiwa kwa bidhaa zinazoingia na kutoka nchini kupitia Bandari ya Dar es Salaam.

Alisema kuwa, licha ya kuongezeka kwa mapato yatokanayo na forodha, bado kuna changamoto ya ukwepaji kodi kupitia mizigo ya transit (inayosafirishwa kwenda nje ya mipaka ya Tanzania).

Mhe. Balozi Omar alieleza kuwa baadhi ya mawakala wasio waaminifu hutumia mwanya huo kuingiza mizigo wakidai inaelekea nchi jirani, lakini baadaye huishusha na kuisambaza ndani ya nchi kinyume cha taratibu yaani “dumping”.
Aidha, aliitaka TRA kuimarisha ushirikiano na nchi zenye uhusiano mkubwa wa kibiashara na Tanzania, ikiwemo China, India na nchi za Umoja wa Nchinza Falme za Kiarabu UAE, akisisitiza umuhimu wa hatua hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho China imeondoa ushuru wa forodha kwa baadhi ya bidhaa zinazoingia nchini humo kutoka barani Afrika.

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda, ameahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na Mhe. Waziri wa Fedha ili kuongeza ufanisi na uwazi katika ukusanyaji wa mapato.
Katika kuimarisha udhibiti wa mizigo ya transit, TRA kupitia ving’amuzi na kamera maalum zinazofungwa kwenye magari ya mizigo kwa lengo la kufuatilia safari na kubaini udanganyifu wa taarifa kuhusu mahali ilipo mizigo, idara hiyo imefanikiwa kukamata matukio 16 ya ukiukwaji huo wa Sheria za nchi (dumping), zenye thamani ya shilingi bilioni 3.2 makosa ambayo 15 kati ya hayo, TRA iliyatoza faini ya shilingi bilioni 2.5, na shauri moja lililokuwa mahakamani, linaendelea kushughulikiwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here