Tume ya Uchunguzi yakutana na Waziri wa Mambo ya Nje

DAR-Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 imekutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Mahmoud Thabit katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam, Februari 17, 2026.
Mkutano huo ambao umefanyika katika ukumbi wa Tanganyika uliopo jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini hapa, ni sehemu ya juhudi za Tume hiyo kukusanya taarifa, maoni na ushauri kutoka kwa viongozi mbalimbali.
Pamoja na mambo mengine, hoja zilizojadiliwa katika mkutano huo zilihusu maeneo ya tathmini ya athari za matukio hayo ndani ya nchi na kimataifa na ushauri wa hatua za kijamii na kisheria zinazochukuliwa ili kuimarisha amani, mshikamano wa kitaifa na kimataifa.
Tume inaendelea kukutana na makundi mbalimbali ikiwemo waathirika wa matukio ya uvunjifu wa amani, kwa lengo la kukusanya ushahidi na taarifa zitakazoiwezesha kuandaa ripoti ya kina.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here