Dkt.Yonazi akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa TACAIDS,Dkt.Adam Joseph Mrisho

DODOMA-Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu,Dkt. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS),Dkt. Adam Joseph Mrisho ambaye amefika kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kikao hicho kimefanyika tarehe 23 Machi, 2026 katika Ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo mtaa wa Reli jijini Dodoma na kudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu),Dkt.James Kilabuko pamoja na Mratibu wa Masuala ya UKIMWI,Bi.Adela Mpina.
Dkt.Yonazi ameahidi kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here