Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linafanya uchunguzi wa kina baada ya kugundua mwili wa Lilian Danstan Manga (27) ukiwa umefukiwa ndani ya nyumba aliyokuwa akiishi na rafiki yake wa kiume katika Kijiji cha Changarawe, Wilayani Kilosa.
Mwili huo ulipatikana baada ya mwanamke aliyekuwa akifanya usafi kubaini uwepo wa tuta la udongo ndani ya chumba cha nyumba hiyo ambayo ilikuwa haijakaliwa kwa miezi kadhaa. Lilian alikuwa ameripotiwa kutoweka tangu Disemba 11, 2025.
Baba wa marehemu, Danstan Albano Manga, ameelezea huzuni kubwa iliyoikumba familia yake baada ya kumtafuta binti yao kwa muda mrefu bila mafanikio.
Tukio hilo limeacha majirani na wakazi wa Kijiji cha Changarawe katika hali ya mshtuko na mshangao mkubwa, huku uongozi wa kijiji ukishirikiana na vyombo vya dola tangu hatua za awali za ugunduzi wa mwili huo ili kuhakikisha haki inatendeka.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, amefika eneo la tukio na kushuhudia zoezi la kufukuliwa kwa mwili huo huku akitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa polisi.
Serikali imeahidi kufuatilia tukio hilo kwa ukaribu ili kubaini chanzo cha mauaji hayo na kumkamata mtuhumiwa anayehusika. Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa rafiki wa kiume wa marehemu ambaye anahisiwa kuhusika na tukio hilo la kikatili.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo
.jpeg)













.jpeg)
.jpeg)







