Mahakamani kwa makosa ya rushwa

MANYARA-Februari 27,2026 katika Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara limefunguliwa shauri la Uhujumu Uchumi Namba 4344/2026 mbele ya Mheshimiwa Charles Uisso,Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya hiyo dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Kituo cha Afya Zahanati ya Sukuro,Bw.David Samson Ndagala.
Mshtakiwa anashtakiwa kwa makosa ya ufujaji na ubadhirifu kinyume na kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura ya 329 R.E 2023, kikisomwa pamoja na aya ya 21 jedwali la kwanza kifungu cha 57(1) na 60(2) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi na makosa ya kupangwa Sura ya 200 R:E 2022.

Aidha, mshtakiwa anashtakiwa kwa kosa la Uchepuzi Kinyume na kifungu cha 29 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Sura ya 329, marejeo ya mwaka 2023), kikisomwa pamoja na aya ya 21 ya Jedwali la Kwanza na vifungu vya 57(1) na 61(2) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi na Makosa ya Kupangwa [Sura ya 200,marejeo ya mwaka 2023].

Akisoma hati ya mashtaka,Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), Bw.Gervas Sarakikya ameiambia Mahakama kuwa mshtakiwa, Daud Samson Ndagala, wakati akitekeleza majukumu yake kama mkuu wa zahanati ya Sukuro, alijipatia isivyo halali fedha kiasi cha shilingi 1,083,000, fedha zilizokuwa chini ya usimamizi wake kutokana na nafasi yake, fedha hizo zikitokana na mauzo ya mifuko 57 ya saruji iliyokuwa imekusudiwa kwa ukarabati wa zahanati hiyo.

Aidha, imeelezwa kuwa, mshtakiwa huyo pia aliitumia mali ya Zahanati ya Sukuro kinyume cha madhumuni yaliyokusudiwa kwa kuhamisha matofali 220 na kumpa mtu mwingine, mali ambayo ilikuwa mikononi mwake kutokana na nafasi yake ya kazi.

Mshtakiwa amekana kutenda makosa yote yanayomkabili na shauri limehairishwa hadi 02/03/2026 kwa ajili ya kusikilizwa hoja za awali (PH).

Kwa sasa mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja ambapo amesaini bondi ya shilingi 1,000,000.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here