Mashindano ya Qurani Tukufu yanaiweka Tanzania kwenye ramani ya Dunia-Rais Dkt.Mwinyi

DAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema, Mashindano Makubwa ya Kimataifa ya Quraan Tukufu kwa mabara yote duniani yameendelea kuwa chachu ya kuimarisha mapenzi ya Quraan, kujenga maadili kwa vijana na kuiweka Tanzania katika ramani ya kimataifa kwa heshima ya kuandaa mashindano kwa kiwango cha juu.
Amesema hayo Machi 1, 2026 katika mashindano yaliyofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, yaliyoandaliwa na Al Hikma Foundation, yakihusisha washiriki kutoka mabara mbalimbali duniani.
Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza kuwa, mashindano hayo si jukwaa la ushindani pekee, bali ni sehemu ya kuimarisha heshima ya taifa, kuendeleza misingi ya Tajweed na Hifdh kwa viwango vya kimataifa, pamoja na kulea kizazi chenye maadili na imani thabiti.

Washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Quraan Tukufu 2026;

1. Abdulrahman Yasin, Uganda – 97% – USD 12,000

2. Mohamed Mustafa, Canada – 96.5% – USD 8,000

3. Shueyb Mohamed, Sweden – 96.2% – USD 5,000

4. Bilal Ahmad, Réunion – 95% – USD 4,000

5. Bilal Hassen, New Zealand – 94.5% – USD 3,000

Rais Dkt. Mwinyi amewapongeza washiriki wote kwa ustadi wao mkubwa, akibainisha kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya juhudi binafsi, malezi bora ya walimu na msaada wa familia.
Amehimiza jamii kuendelea kuisoma, kuielewa na kuifanyia kazi Quraan kama nuru na mwongozo wa maisha ya kila siku ili kujenga taifa lenye mshikamano na maadili mema.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Viongozi wa Dini, Serikali, Mabalozi, Wanazuoni wa Kiislamu na Maelfu ya Wananchi waliojitokeza kushuhudia tukio hilo la kihistoria lenye hadhi ya kimataifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here