Mwalimu wa Shule ya Msingi Mwamkulu afariki kwa kushambuliwa na myama mkali

KATAVI-Mwalimu wa Shule ya Msingi Mwamkulu, Hamad Aidan (50) amefariki dunia kufuatia tukio linalodaiwa kuhusisha shambulio la mnyama mkali katika Kijiji cha Mwajuni, Tarafa ya Misunkumilo iliyopo Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Kamishna Msaidizi wa Polisi (SACP) Kaster Ngonyani, marehemu aliondoka nyumbani kwake mnamo Machi 18, 2026, baada ya kumuaga mke wake, Malia Azeri (47) akielekea shuleni kwa shughuli zake za kila siku.

Hata hivyo, Machi 20,2026 majira ya saa 4:00 asubuhi, mwili wake ulikutwa ukiwa na majeraha katika sehemu mbalimbali za mwili, hali iliyoashiria kuwa tayari alikuwa amefariki dunia.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa,tukio hilo linaweza kuwa limetokana na kushambuliwa na mnyama mkali.

Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi, huku uchunguzi wa kina ukiendelea kubaini ukweli kamili wa tukio hilo.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limetoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zozote zitakazosaidia kufanikisha uchunguzi huo, ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here