Rais Dkt.Mwinyi aipongeza Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa matibabu ya kibingwa

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameipongeza Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma kwa mageuzi na mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma za matibabu ya kibingwa kwa wananchi.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Machi 4,2026 alipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Prof. Abel Makubi, akiambatana na ujumbe wake, waliofika Ikulu, Zanzibar.

Rais Dkt. Mwinyi amesifu hatua kubwa ya utoaji wa huduma za kibingwa, ikiwemo matibabu ya figo, moyo na ubongo kufanyika nchini, hatua aliyoielezea kuwa imeipunguzia Serikali na wananchi gharama za kuwapeleka wagonjwa kutibiwa nje ya nchi.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameuishauri uongozi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kuendeleza utaratibu wa matibabu ya nje kwa kuwafikia wananchi katika maeneo yao kupitia mpango wa outreach programme, kwani unasaidia kuwatibu watu wengi zaidi.

Rais Dkt. Mwinyi ameahidi kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kupitia Wizara ya Afya Zanzibar, itaendeleza ushirikiano na Hospitali ya Benjamin Mkapa na kutafuta njia bora zaidi za kufanya kazi kwa pamoja.
Pia, ameipongeza hospitali hiyo kwa kuendeleza mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji kupitia taasisi za ndani na wadau kutoka nje ya nchi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Prof. Abel Makubi, ameeleza kuwa hospitali hiyo imepata mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake kwa kutoa huduma za matibabu bobezi na kibingwa zaidi ya 20, ikiwemo upandikizaji wa figo, upasuaji wa ubongo na matibabu ya moyo, hali iliyochangiwa na jitihada za Serikali kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya afya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here