Serikali itaendelea kushirikiana na TTCL kuimarisha mawasiliano Zanzibar-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL),David Nchimbi aliyeambatana na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, CPA Moremi Marwa, pamoja na ujumbe wao waliofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha Machi 23,2026.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameahidi kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na shirika hilo katika kuimarisha mawasiliano Zanzibar kupitia huduma mbalimbali zinazotolewa na TTCL.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL,David Nchimbi amemshukuru Rais Dkt.Mwinyi kwa ushirikiano unaoendelea kati ya shirika hilo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha huduma za mawasiliano nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here