TANESCO kufanya maboresho ya Mfumo wa Manunuzi ya Umeme (LUKU)

NA DIRAMAKINI

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limewataarifu wateja wake kuwa litafanya maboresho ya mfumo wa manunuzi ya umeme wa kulipia kabla (LUKU), hatua inayolenga kuboresha ufanisi na upatikanaji wa huduma hiyo kwa watumiaji.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika hilo leo Machi 10,2026 maboresho hayo yanatarajiwa kufanyika kesho Jumatano usiku kuamkia Alhamisi kuanzia saa 6:00 usiku hadi saa 8:00 usiku, sawa na muda wa masaa mawili.

Kutokana na zoezi hilo la kiufundi, huduma ya kununua umeme kupitia mfumo wa LUKU haitapatikana katika kipindi chote cha maboresho hayo.

Aidha, TANESCO imewashauri wateja wake kununua umeme mapema kabla ya muda uliopangwa wa maboresho ili kuepusha usumbufu wowote unaoweza kujitokeza wakati huduma hiyo itakapokuwa imesitishwa kwa muda.

Shirika hilo limeeleza kuwa, maboresho hayo ni sehemu ya juhudi zake za kuimarisha mifumo ya utoaji huduma kwa wateja na kuhakikisha upatikanaji wa huduma za umeme unakuwa bora na wa kuaminika zaidi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here