Tume ya Jaji Chande kuimarisha demokrasia

GENEVA-Serikali imeihakikishia jumuiya ya kimataifa kuwa, matokeo ya Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Oktoba 29, mwaka jana, yataongeza uwajibikaji, umoja na maridhiano nchini Tanzania.
Pia, Serikali imesisitiza Tume hiyo chini ya Jaji Mohamed Chande, iko huru katika kazi zake hatua ambayo italeta matokeo makubwa na chanya.

Akiwasilisha mada katika Kikao cha 61 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC), mjini Geneva, Uswisi, juzi, Mkurugenzi Msaidizi wa Taarifa za Haki za Binadamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Beatrice Mpembo, alisema uamuzi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuunda Tume hiyo umelenga kuweka uwazi, imani ya wananchi na uwajibikaji kwa kuangalia matukio yote ya Oktoba 29, mwaka jana, baada ya Uchaguzi Mkuu.

Beatrice alifafanua, Novemba 18, mwaka jana, Rais Samia aliunda Tume hiyo kwa mujibu wa Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32, kwa lengo la kupata undani wa matukio ya Oktoba 29, chanzo na kilichoendelea baada ya kuibuka vurugu.

"Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hasaan, aliunda Tume kama chombo huru, maalumu cha uchunguzi na usimamizi kwa lengo la kuishauri serikali hatua zinazopaswa kuchukuliwa," alifafanua Beatrice.
Aliongeza, Tume hiyo inachunguza visababishi, madai ya vijana, vitendo vya upinzani, kuona kama kulikuwa na ufadhili wa vurugu kutoka nje na kuthamini kazi ya vyombo vya usalama katika kuleta utulivu wakati wa vurugu hizo.

MATARAJIO

Alifafanua, matokeo ya Tume yataimarisha amani, utulivu, kuponya mpasuko wa kijamii, kuleta majadiliano ya kitaifa, kushughulikia malalamiko ya kihistoria, kuzuia migogoro, kuimarisha utawala wa kidemokrasia na umoja wa kitaifa.

Tayari serikali imekwishachukua hatua madhubuti ikiwemo msamaha kwa vijana 1,787 waliohusika katika matukio ya Oktoba 29, kwa kushawishiwa na kuunda Wizara maalumu ya Vijana.

Tume ya Jaji Chande inaheshimika kimataifa kutokana na rekodi ya Mwenyekiti huyo katika anga za haki za binadamu na sheria za kimataifa, ilipewa kazi kwa siku 90 baadaye ikaongezewa siku 42 hadi mwezi ujao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here