Zaidi ya shilingi bilioni 127.7 zimetumika kupeleka huduma ya nishati safi Vijijini Mkoa wa Mwanza hali iliyochochea ukuaji wa uchumi na kuboreka kwa huduma za kijamii vijijini.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda wakati wa kikao cha kwanza kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wabia wa Maendeleo katika Sekta ya Nishati (EDPG) ambapo Wakala huo uliwasilisha mpango kazi pamoja na bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2026/2027.“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkoa wa Mwanza pekee imetoa jumla ya shilingi Bilioni 127.7 ili kutekeleza miradi ya kupeleka umeme hadi vitongojini. Mafanikio haya makubwa yamechangiwa pia na wabia wa maendeleo, tunawapongeza na kuwashukuru sana.
"Niendelee kuwataka wananchi waendelee kulinda miundombinu ya umeme kwa kuwa serikali na wabia hawa wa maendeleo wanaweka fedha nyingi sana. Lakini pia niendelee kuwahimiza wabia wa maendeleo pamoja na REA kuendelea kuwekeza zaidi katika nishati safi ya kupikia,” amesema Mhe. Mtanda.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo























