Mama Mariam Mwinyi awatembelea wakulima wa mwani, asisitiza thamani ya masoko ya zao hilo

ZANZIBAR-Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mhe. Mama Mariam Hussein Mwinyi, amewatembelea wakulima wa mwani pamoja na wanufaika wa mradi katika eneo la Muungoni, Wilaya ya Kusini Unguja, Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 16 Aprili 2026, chini ya Programu ya Pamoja ya Kuwezesha Wanawake wa Vijijini Kiuchumi (Joint Programme on Rural Women’s Economic Empowerment – JP RWEE).
Katika ziara hiyo, Mhe. Mama Mariam Hussein Mwinyi ameambatana na wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya ZMBF, ambapo alipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na wanufaika wa programu hiyo pamoja na hatua za maendeleo zilizofikiwa.
Akizungumza na wakulima hao, Mhe. Mama Mariam Hussein Mwinyi ameeleza kufurahishwa na maendeleo yanayoonekana, akibainisha kuwa mafunzo yaliyotolewa yameanza kuzaa matunda.

Amesema kuwa hatua hiyo imechangia kuongezeka kwa uzalishaji na kuboreshwa kwa ubora wa mwani ikilinganishwa na hali ya awali.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuendeleza juhudi za kuwajengea uwezo wakulima kwa kuwapatia mafunzo endelevu, sambamba na kuanzisha mbinu bunifu za uchakataji wa mwani ili kuongeza thamani ya zao hilo.
Aliongeza kuwa,hatua hizo zitasaidia kuboresha masoko, kuongeza bei ya mauzo na hatimaye kuinua kipato cha wakulima.

Vilevile, Mhe. Mama Mwinyi Mwinyi amebainisha kuwa programu hiyo inaendelea kuwa chachu muhimu katika kuwawezesha wanawake wa vijijini kiuchumi, kukuza ajira endelevu na kuimarisha mchango wa sekta ya mwani katika kukuza uchumi wa buluu Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here