TRC Yang’ara:Treni ya umeme yawa mkombozi wakati wa msukosuko wa uchumi duniani

KATIKA kipindi ambacho dunia imekumbwa na changamoto za kiuchumi zinazochangiwa kwa kiasi kikubwa na mgogoro wa Mashariki ya Kati unaoendelea sasa, sekta nyingi za usafirishaji zimejikuta zikitetereka.
Kupanda kwa bei ya mafuta kumeathiri moja kwa moja gharama za uendeshaji, na kusababisha baadhi ya watoa huduma katika nchi mbalimbali, kulazimika kuongeza nauli ili kuendana na hali hiyo.

Hata hivyo, nchini Tanzania hali imekuwa tofauti. Kupitia uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeendelea kutoa huduma ya uhakika kupitia treni ya kisasa ya umeme (SGR), ambayo haitegemei mafuta.
Hili limeifanya sekta ndogo ya reli Tanzania kuwa katika nafasi ya kipekee ya kukabiliana na athari za msukosuko wa bei ya nishati duniani.

Sauti za abiria zimekuwa zikisikika wazi, zikionesha kuridhishwa na huduma hii. Wengi wanapongeza TRC kwa ubunifu na ufanisi wake, huku wakitoa shukrani za dhati kwa Serikali kwa maamuzi ya kimkakati yaliyowezesha uwepo wa reli ya umeme, kwao, treni hii si tu njia ya usafiri, bali ni suluhisho la gharama nafuu na uhakika katika nyakati ngumu kama hizi.

Abiria wengi wameeleza kuwa wakati nauli za usafiri mwingine zikiongezeka, huduma ya SGR imeendelea kuwa nafuu na thabiti, jambo linalowapa unafuu mkubwa wananchi wa kipato cha chini na cha kati.
Aidha, uhakika wa muda, usalama, na utulivu vinavyoambatana na safari za treni hii vimeongeza thamani yake kwa watumiaji.

Mafanikio haya ni ushahidi thabiti wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya kisasa na endelevu hususani ya usafiri na usafirishaji.

Uamuzi wa kuwekeza katika reli ya umeme unaonekana sasa kuwa wa busara zaidi, hasa ukizingatia changamoto za nishati zinazoikumba dunia.

Kwa ujumla, TRC imejidhihirisha kuwa mhimili muhimu katika kuimarisha uchumi wa Taifa na kupunguza athari za misukosuko ya kimataifa kwa wananchi, aidha ni dhahiri kuwa uwekezaji huu unaendelea kuzaa matunda, na kuifanya Tanzania kusonga mbele kwa kasi katika safari yake ya maendeleo.

Imeandaliwa na
Fredy Mwanjala,
Mkuu wa Kitengo cha Uhuasiano na Mawasiliano,
Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here