Wizara ya Nishati yapanga kuimarisha upatikanaji wa umeme na nishati safi 2026/27, yaomba shilingi trilioni 2.5

NA GODFREY NNKO

WIZARA ya Nishati imeliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha jumla ya shilingi trilioni 2.525 kwa ajili ya matumizi ya wizara ya hiyo na taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Hayo yameelezwa leo Aprili 22,2026 na Waziri wa Nishati, Mheshimwa Deogratius Ndejembi wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo bungeni jijini Dodoma.

Ameeleza kuwa, kati ya fedha hizo, asilimia 97.5 sawa na Shilingi trilioni 2.462, zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo. 

Kati ya fedha hizo za maendeleo, Shilingi trilioni 1.602 ni fedha za ndani, huku Shilingi bilioni 859.9 zikiwa ni fedha za nje.

Kwa upande wa matumizi ya kawaida, Waziri huyo amesema, jumla ya Shilingi bilioni 63.03, sawa na asilimia 2.5 ya bajeti yote, zimetengwa kwa ajili ya kugharamia shughuli za uendeshaji.

Waziri Ndejembi amesema kuwa, katika mwaka wa fedha 2026/27, Wizara yake itaendelea kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa kutosha unaokidhi mahitaji ya ndani pamoja na ziada itakayouzwa nje ya nchi ili kuongeza mapato ya fedha za kigeni.

Ameeleza kuwa, mkakati huo utaenda sambamba na juhudi za kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika maeneo ya mijini, vijijini na vitongojini.

Sambamba na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini ili kulinda mazingira na kuboresha afya za wananchi.

Amefafanua kuwa,wizara pia itaweka mkazo katika shughuli za utafutaji, uendelezaji, uzalishaji na usambazaji wa mafuta na gesi asilia, kwa lengo la kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa bidhaa za mafuta nchini.

Vilevile, Serikali itaendelea kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu ya kuhifadhi na kusambaza rasilimali hizo muhimu kwa maendeleo ya uchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here