Dkt.Maghembe azindua Kongamano la Vijana wa Kitanzania chini ya Umoja wa Mataifa (TIMUN 2026)

ZANZIBAR-Leo tarehe 18 Mei 2026, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt.Ngwaru Jumanne Maghembe (Mb) amemwakilisha Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye uzinduzi wa Kongamano la Vijana wa Kitanzania chini ya Umoja wa Mataifa (Tanzania International Model United Nations-TIMUN 2026) linalofanyika Zanzibar.
Katika hotuba yake, Mhe.Naibu Waziri Dkt. Maghembe amesisitiza umuhimu wa nafasi ya vijana katika kuleta maendeleo endelevu na mabadiliko chanya, kupitia teknolojia, diplomasia na ubunifu katika ngazi na Taifa na Ulimwenguni.
Mkutano wa TIMUN 2026, ni jukwaa muhimu la kimataifa linalolenga kukuza viongozi vijana, wanadiplomasia, wabunifu, na mawakala wa mabadiliko ambalo hufanyika kila mwaka chini ya uratibu wa Chama cha Vijana katika Umoja wa Mataifa Tanzania (Youth of United Nations Association Tanzania-YUNA).

Mhe. Maghembe ameipongeza YUNA Tanzania kwa kuwawezesha vijana na kuendeleza maadili ya Umoja wa Mataifa miongoni mwa vijana wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
"Tumieni mkutano huu kubadilishana mawazo, kujenga ushirikiano, na kuibua suluhisho za changamoto mbalimbali zikiwemo mabadiliko ya tabianchi, ukosefu wa ajira, usawa wa kijinsia, na maendeleo ya teknolojia," amebainisha Mhe.Maghembe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here