Dkt.Natu aongoza ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya makatibu kwenye Mkutano wa 18 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri EAC wanaoshughulikia masuala ya fedha na uchumi

ARUSHA-Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, ameshiriki na kuongoza ujumbe wa Serikali ya Tanzania katika Mkutano wa 18 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaosimamia Masuala ya Fedha na Uchumi - Ngazi ya Makatibu Wakuu, uliofanyika katika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, jijini Arusha, ambao umejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano katika maeneo ya kiuchumi hususan hali ya mwenendo wa viashiria vya Uchumi Mpana kwa Nchi zote wanachama wa Jumuiya, ambayo yatawasilishwa katika Mkutano wa Ngazi ya Mawaziri.
Mkutano huo umehudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elija Mwandumbya, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango anayeshughulikia Mipango ya Kitaifa, Dkt. Mursali Milanzi, na Wataalamu wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here