LIVE:Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo Mei 7,2026 bungeni jijini Dodoma kwa mwaka wa fedha 2026/2027
"Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa ndani ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo iliyochambua na kutoa ushauri wa makadirio ya mapato na matumizi ya FUNGU 46 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na FUNGU 18 - Tume ya Taifa ya UNESCO, sasa ninaomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26.
"Aidha, ninaomba Bunge lako Tukufu likubali kujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2026/27,"Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda leo Mei 7,2026 bungeni jijini Dodoma.