Magazeti leo Mei 11,2026

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kaspar Mmuya ameagiza Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoani Njombe kumkabidhi Charnjeet Singh Sahota hati ya hakimiliki ya Kiwanja Na. 75 Kitalu P mjini Makambako baada ya kubainika kuwa ndiye mmiliki halali wa eneo hilo.
Mmuya alitoa maagizo hayo Mei 9, 2026 katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Polisi Makambako kufuatia mgogoro wa muda mrefu wa ardhi uliodaiwa kuhusisha watu waliotaka kujimilikisha eneo hilo kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Ardhi wa Halmashauri ya Mji Makambako, Flaviana Mamkwe, Charnjeet alirithi eneo hilo kutoka kwa baba yake aliyelinunua kihalali miaka iliyopita.

Ziara ya Mmuya mkoani Njombe imelenga kusikiliza kero za ardhi, kukabidhi hati za hakimiliki na kuhamasisha wananchi kulipa kodi ya pango la ardhi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here