Magazeti leo Mei 5,2026

Mfanyabiashara Rostam Aziz amewataka Watanzania kuacha mtazamo hasi dhidi ya Wakenya, akisema ushindani usio na tija unaweza kudhoofisha fursa za kiuchumi za kikanda.
Akizungumza Mei 4, 2026 katika kongamano la biashara kati ya Tanzania na Kenya lililofanyika Julius Nyerere International Convention Centre jijini Dar es Salaam, Rostam Aziz alisema kuna haja ya kujenga ushirikiano badala ya kuendeleza mitazamo ya hofu kuhusu ajira na uwekezaji.

Pia aliwataka Wakenya kuepuka kufurahia changamoto zinazoikumba Tanzania, akisisitiza umuhimu wa kuheshimiana katika uhusiano wa kikanda.

Kongamano hilo lilihudhuriwa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Rais wa Kenya William Samoei Ruto pamoja na wadau wa biashara.

“Umoja ni nguvu, tunahitaji mfumo mmoja wa biashara unaofanya kazi kwa kasi na ufanisi,” alisema Aziz.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here