Magazeti leo Mei 9,2026

Mahakama ya Wilaya ya Kasulu imemhukumu mshitakiwa Baraka Alphonce Kilisheni (19), mkulima na mkazi wa Mtaa wa Kigamboni, Kabanga Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kifungo cha kwenda jela maisha baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 13.
Mshtakiwa alitenda kosa hilo Septemba 13, 2025 huko Mtaa wa Nyansha Wilayani Kasulu na kufikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Septemba 25,2025.
Akitoa huku hiyo Mei 7,2026 Hakimu Mkazi Mfawidhi Mheshimiwa Imani Batezi amesema kuwa Mahakama imejiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na hatimaye kumtia hatiani mshitakiwa kwa kosa hilo.

Mshitakiwa huyo amehukumiwa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa wahalifu wanaojihusisha na vitendo vya ukiukaji wa sheria,maadili na ukatili wa kijinsia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here