MOROGORO-Wazazi wa mtaa wa Kambitano Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro wametakiwa kuwapinga vikali watoto wao wanaotaka kuacha shule kwa sababu mbalimbali zisizo na tija.
Hayo yamesemwa na Polisi wa Kata ya Lukobe Mkaguzi wa Polisi (INSP) Zuwena Mwita alipokuwa akitoa elimu kwenye moja ya kinamama kinachojulikana kwa jina la Jikwamue.
Katika utoaji huo wa elimu INSP Mwita amesisitiza matumizi sahihi ya mikopo kwa kuwataka wafanye lengo kusudiwa na kuacha tabia ya kutumia pesa kwa kujionyesha hususani kwenye tabia mbalimbali zikiwemo sherehe na tafrija zisizo za lazima.
