Polisi Pwani waokoa ng'ombe 28 wa wizi

PWANI-Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani Mei 22, 2026 huko maeneo ya Tungutungu, Mapinga, Wilayani Bagamoyo, limeokoa jumla ya ng’ombe 28 kati yao ng’ombe 13 ni mali ya Fadhili Ally Ngabilo mkazi wa Kwa Makocho, Kata ya Mandela wilayani Chalinze.
Mei 16, 2026 Bw. Fadhili Ngabilo aliripoti katika kituo cha Polisi Chalinze kuibiwa jumla ya ng’ombe 18 na mbuzi 05 ambapo Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kupitia Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo (STPU) walianza ufuatiliaji mara moja mpaka Mei, 22 majira ya saa 3:00 asubuhi walipofanikiwa kuwapata ng’ombe 28 wakiwemo ng’ombe 13 kati ya 18 walioibiwa Chalinze wakiwa kwenye zizi la mfanyabiashara mmoja wa nyama.
Kati ya ng’ombe wengine 15 waliokutwa nyumbani kwa mtuhumiwa, ng’ombe 5 walitambulika na ng’ombe 4 mahojiano yanaendelea.

Aidha ilibainika mtuhumiwa huyo huwa anachinja ng’ombe wa wizi nyumbani hapo kisha kuuza nyama kwenye bucha yake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Salim Morcase alieleza kuwa mpaka sasa jumla ya watuhumiwa wanne wanashikiliwa na mara baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani.
Aidha, alitoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa sahihi kwa kadri operesheni za kudhibiti uhalifu zinavyofanyika maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa wa Pwani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here