Rais Dkt.Mwinyi ashiriki dua ya kumuombea Sheikh Abuubakar Al-Abassy, atoa pole kwa familia ya Waziri Nadir Al-Wardi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika dua maalum ya kumuombea marehemu Sheikh Abuubakar bin Said Al-Abassy.
Dua hiyo imesomwa leo Mei 2,2026 katika Ukumbi wa Majid uliopo Kiembe Samaki, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais Dkt. Mwinyi amemuelezea mwanazuoni huyo kuwa alikuwa mtu mwema, mwenye upendo, na aliyewafundisha watu wengi elimu ya dini.

Wakati huohuo, Rais Dkt. Mwinyi ametoa mkono wa pole kwa Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mhe. Nadir Abdullatif Al-Wardi, pamoja na familia yake kufuatia kifo cha baba yao mzazi aliyefariki nchini India.
Rais Dkt. Mwinyi alifika nyumbani kwa familia hiyo, Chukwani Buyu, kutoa mkono wa pole na kuwataka kuwa na subira katika kipindi hiki cha msiba mzito.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here