TAKUKURU Pwani kwa kushirikiana na Manispaa ya Kibaha yapaisha makusanyo,yawezesha shilingi bilioni 1.6 zilizokuwa zinapotea kukusanywa

PWANI-Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na Manispaa ya Kibaha imefanikiwa kuzuia upotevu wa mapato na kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 1.6 zilizokuwa zinapotea kupitia ushuru wa huduma, baada ya kubaini baadhi ya wafanyabiashara wakifuta stakabadhi za mauzo na kukwepa kulipa kodi stahiki.
Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani, Ezekia Sinkara, amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2026.

Amefafanua kuwa,katika ufuatiliaji uliofanywa kwa kushirikiana na Manispaa ya Kibaha, TAKUKURU ilibaini uwepo wa mbinu mbalimbali zilizokuwa zikitumiwa na baadhi ya wafanyabiashara kukwepa ushuru wa huduma, ikiwemo kufuta stakabadhi za mauzo ambazo tayari zilikuwa zimefanyika ili kupunguza kiwango halisi cha mauzo.
“Tumebaini baadhi ya wafanyabiashara wakifanya biashara bila kutoa risiti za EFD, hususan katika maduka ya jumla pamoja na biashara za bidhaa zitokanazo viwandani,” amesema Sinkara.

Aidha, amesema baadhi ya kampuni zilikuwa zikihamisha bei za bidhaa kutoka kampuni mama kwenda kwenye matawi yake kwa lengo la kupunguza kiwango cha mauzo kinachoonekana na hivyo kukwepa kulipa ushuru unaostahili.

Kwa mujibu wa Sinkara, hatua za uzuiaji zilizochukuliwa na TAKUKURU kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha zimeongeza ukusanyaji wa mapato katika halmashauri hiyo.
Amesema,katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha, mapato yaliyokusanywa yalifikia shilingi bilioni 1.5, robo ya pili yakafikia bilioni 1.8 huku robo ya tatu ikifikia bilioni 1.6. Katika robo hii ya tatu zoezi linaendelea na kufanya jumla ya makusanyo kufikia shilingi Bilioni 4.9

Sinkara amesema,TAKUKURU itaendelea kushirikiana na mamlaka mbalimbali za serikali kuhakikisha mianya ya upotevu wa mapato inazibwa na wahusika wanaobainika kuchukua hatua zinazokiuka sheria wanachukuliwa hatua stahiki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here