TMA yatoa angalizo la mvua maeneo mbalimbali nchini

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa siku kumi kuanzia Mei 1 hadi Mei 10, ikionyesha kuwa mvua zitaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Maeneo yatakayoathirika zaidi ni Ukanda wa Ziwa Victoria, ukanda wa pwani, pamoja na baadhi ya sehemu za nyanda za juu kaskazini.

Katika mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara, mvua zinatarajiwa kuambatana na radi katika maeneo kadhaa.

Kwa upande wa kaskazini-mashariki (Arusha, Manyara na Kilimanjaro), kunatarajiwa mvua nyepesi katika maeneo machache, huku hali ya unyevunyevu ikiendelea katika ukanda wa pwani.

Mikoa ya Tanga, kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, inatarajiwa kupata mvua zitakazoambatana na radi katika baadhi ya maeneo.

Magharibi mwa nchi, ikiwemo Kigoma, Katavi na Tabora, kutakuwa na mvua za hapa na pale pamoja na radi chache.

Hata hivyo, hali ya ukame itaendelea katika ukanda wa kati, hasa Dodoma na Singida. Katika nyanda za juu kusini-magharibi na maeneo ya kusini, mvua nyepesi na za vipindi zinatarajiwa kunyesha katika baadhi ya maeneo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here