Tuliteseka sana kufanya biashara katika mazingira yasiyo rafiki,tunamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kumtuma Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu kuja Kibakwe kutufungulia soko letu jipya la mazao

DODOMA-Wananchi wa Kibakwe mkoani Dodoma wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea soko jipya la mazao litakaloboresha mazingira ya biashara na kuinua shughuli za kiuchumi katika eneo hilo.
Wakizungumza mara baada ya uzinduzi wa soko hilo, wananchi hao wamesema hapo awali walikuwa wakifanya biashara katika mazingira yasiyoridhisha yaliyokuwa yakikabili shughuli zao za kila siku.

Wameeleza kuwa,ujenzi wa soko hilo ni hatua muhimu itakayowezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwa utulivu,usalama na ufanisi zaidi.

Aidha, wananchi hao wamemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kumtuma Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba kufika Kibakwe kwa ajili ya kushiriki katika uzinduzi wa soko hilo jipya la mazao.

Soko hilo ambalo limefunguliwa na Waziri Mkuu linatarajiwa kuwa na uwezo wa kuhudumia wafanyabiashara kati ya 300 hadi 350 kwa wakati mmoja, hatua inayotarajiwa kuongeza fursa za biashara na kukuza uchumi wa wananchi wa eneo hilo na maeneo jirani.

Wananchi wameeleza kuwa,mradi huo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuendelea kuboresha huduma na miundombinu ya biashara nchini, huku wakisisitiza kuwa maendeleo hayo yameendelea kuleta matumaini mapya kwa jamii.

“Kwa kweli tabasamu linaendelea kutokana na maboresho haya makubwa yanayotekelezwa na Serikali,” alisema mmoja wa wananchi waliohudhuria hafla hiyo.
Mei 9,2026 akizungumza na wananchi baada ya uzinduzi wa soko hilo, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amejitambulisha kuwa kiongozi wa matokeo kwa kutekeleza miradi mbalimbali inayogusa moja kwa moja maisha ya Watanzania.

“Mheshimiwa Dkt. Samia ni mtendaji. Ambaye akisema jambo, anatekeleza. Na haya yanadhihirishwa kwa kazi kubwa ambayo imefanyika.”

Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amefanya kazi kubwa inayowapa heshima Watanzania wote. “Nchi inapopiga hatua, kwa kazi kubwa inayofanywa Rais wetu, inalinda heshima ya uhuru wa nchi.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here