Vijana wahimizwa kuimarisha usalama na kudumisha amani katika jamii zao

KIGOMA-Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limetoa wito kwa vijana kata ya Buhigwe, Wilaya ya Buhigwe, Mkoa wa Kigoma kushiriki kuimarisha usalama maeneo wanayoishi kwa kufanya doria kupitia vikundi vya ulinzi shirikishi.
Wito huo umetolewa Mei 9,2026 na Mkaguzi wa Polisi (INSP) Mhadham Miyonga wakati akitoa elimu ya umuhimu wa vikundi vya ulinzi shirikishi katika kuimarisha usalama ambapo amewataka vijana kushiriki kuimarisha usalama maeneo wanayoishi kwa kufanya doria kupitia vikundi vya ulinzi shirikishi, wasione jukumu hilo ni la kundi la wazee ndani ya jamii bali hata wao wanawajibu kushiriki kuimarisha usalama.

INSP Miyonga amewataka vijana hao kuendelea kulinda amani ndani ya jamii kwa kutoa taarifa za wahalifu na kutoshiriki vitendo vya uvunjifu wa amani.

Pamoja na hayo amewataka vijana hao kutojihusisha na matumzi ya dawa za kulevya kwa usalama wa afya zao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here