DAR-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mkuu Mtendaji wa Perseus Mining Limited, Bw. Craig Jones, aliyeambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Fedha wa kampuni hiyo Bi. Lee-Anne de Bruin, pamoja na Meneja Mkazi wa Kampuni ya Sotta Mining Corporation Limited, Bw. Isaac Lupokela, katika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano katika kukuza sekta ya madini pamoja na uwekezaji.



