DAR-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Habib African, Bw. Faraz Haider, aliyeambatana na Mwenyekiti wake wa Bodi anayemaliza muda wake, Bw. Zain Habib, katika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaaam, ambapo wamezungumza fursa mbalimbali zilizopo nchini hasa katika uwekezaji katika ujenzi wa nyumba za makazi za bei nafuu katika miji inayokua kwa kasi nchini.








