Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora,SACP Richard George Abwao azikwa Shirati

NA DIRAMAKINI

ALIYEKUWA Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Richard George Abwao amezikwa rasmi Ijumaa ya Juni 26, 2026 katika Kijiji cha Shirati, Wilaya ya Rorya mkoani Mara, huku maelfu ya waombolezaji wakijitokeza kumpa heshima za mwisho.
Maziko hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Jeshi la Polisi,ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali waliofika kuungana na familia katika kuaga mmoja wa viongozi waliolitumikia Jeshi la Polisi kwa kipindi kirefu.

Kabla ya kuzikwa, mwili wa marehemu uliagwa kwa heshima jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi na watumishi wa Jeshi la Polisi pamoja na wananchi walipata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho.
Baadaye, ibada maalumu ya kuuaga mwili ilifanyika nyumbani kwa marehemu mkoani Morogoro kabla ya mwili kusafirishwa kuelekea mkoani Tabora kwa ajili ya kuagwa na wananchi na viongozi wa eneo alilokuwa akilihudumia na hatimaye kupelekwa mkoani Mara kwa maziko.

Marehemu Richard Abwao alifariki dunia Juni 20, 2026 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Kifo chake kimeacha pengo kubwa ndani ya Jeshi la Polisi na kwa wananchi aliowahudumia katika maeneo mbalimbali ya nchi, ambapo ameelezwa kuwa alikuwa kiongozi aliyekuwa na weledi, nidhamu na aliyesimamia kikamilifu utekelezaji wa majukumu yake ya kulinda usalama wa raia na mali zao.
Waombolezaji waliohudhuria maziko hayo walielezea masikitiko yao kwa kuondokewa na kiongozi huyo, wakisema mchango wake katika kuimarisha ulinzi na usalama utaendelea kukumbukwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here