BoT yawanoa wanafunzi wa UDSM kuhusu elimu ya fedha

DAR-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeendesha mafunzo maalum kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu majukumu ya Benki Kuu pamoja na masuala ya elimu ya fedha.
Katika mafunzo hayo yaliyofanyika tarehe 24 Juni 2026, wanafunzi hao walipatiwa elimu kuhusu jukumu kuu la BoT la kuandaa na kutekeleza sera ya fedha inayolenga kudhibiti mfumuko wa bei, kuhakikisha utulivu wa mfumo wa fedha na kuchangia ukuaji endelevu wa uchumi wa taifa.
Aidha, wanafunzi hao walielimishwa kuhusu fursa za uwekezaji katika dhamana za Serikali, ikiwemo hati fungani za muda mfupi na muda mrefu, ambazo usimamizi na uratibu wake hufanywa na BoT.

Mafunzo hayo pia yalihusisha mada za usimamizi binafsi wa fedha, zikiwemo umuhimu wa kuweka akiba, kupanga bajeti na kujiandaa kwa maisha ya kujitegemea baada ya kuhitimu masomo yao.
BoT inaendelea kutekeleza programu mbalimbali za elimu kwa umma kwa lengo la kuongeza uelewa wa masuala ya fedha na uchumi, pamoja na kuimarisha ushirikiano na taasisi za elimu nchini ili kuwezesha wananchi, kufanya maamuzi sahihi ya kifedha na kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here