Mheshimiwa Wanu asisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali,sekta binafsi na taasisi za elimu katika kuwaandaa vijana kwa soko la ajira

DAR-Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi na taasisi za elimu katika kuwaandaa vijana kwa soko la ajira kupitia mafunzo yanayozingatia mahitaji halisi ya sasa.
Mhe. Wanu ametoa rai hiyo Juni 6, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake katika Kiwanda cha Superdoll, ambapo amehimiza utoaji wa elimu inayojikita katika ujuzi na umahiri ili kuwajengea wahitimu uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi na kuendana na mahitaji ya sekta za uzalishaji.

Mhe. Ameir ameeleza kuwa Serikali inaendelea na ujenzi wa vyuo 105 vya VETA na kuboresha vingine 12, hatua inayolenga kuongeza upatikanaji wa mafunzo ya ufundi stadi na kuwawezesha vijana kupata ujuzi unaohitajika katika uchumi unaobadilika.

Mhe. Wanu ameendelea kuzihimiza taasisi na wadau wengine kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kufungua milango ya mafunzo ya vitendo kwa vijana na wakufunzi ili kupunguza pengo kati ya maarifa ya darasani na ujuzi unaohitajika sokoni.

Aidha, ameitaka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuharakisha utiaji saini wa makubaliano na Kampuni ya Superdoll ili kuimarisha zaidi mafunzo ya vitendo kwa vijana.
Meneja wa Superdoll Bw. Ibrahim Ali amesema kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana kwa karibu na taasisi za elimu, hususan VETA, ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa mafundi wake, huku takribani asilimia 80 ya mafundi wa kampuni hiyo wakiwa wahitimu wa VETA. Ameongeza kuwa hivi karibuni kampuni imepokea vijana 20 kwa ajili ya tawi lake la Dodoma.
Naibu Waziri ameiagiza Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kutambuliwa rasmi Kituo Maalumu cha Mafunzo (Center of Excellence) cha Superdoll katika kukuza ujuzi na kuongeza uzoefu wa kazi kwa vijana wa Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here