Rais Dkt.Mwinyi aitaka jamii kushirikiana mapambano dhidi ya dawa za kulevya na kuimarisha malezi bora

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesisitiza umuhimu wa jamii kuunganisha nguvu katika kupambana na matumizi ya dawa za kulevya kwa kuimarisha malezi bora ya watoto na vijana, ili kulinda nguvu kazi na mustakabali wa Taifa.
Rais Dkt. Mwinyi ametoa wito huo leo Juni 26,2026, aliposhiriki Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al Azhar, Mpendae, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amesema,malezi bora yanayoanzia ndani ya familia na kuzingatia mafunzo ya dini ndiyo msingi wa kujenga vijana wenye maadili na kuwakinga dhidi ya dawa za kulevya,uhalifu na vitendo vingine viovu.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesema maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Matumizi Mabaya na Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya yatakayofanyika tarehe 27 Juni yanapaswa kuwa chachu ya kuongeza uelewa na ushiriki wa jamii katika kutokomeza tatizo hilo.

Katika kuadhimisha siku ya Ashura, Rais Dkt. Mwinyi amewahimiza waumini kuongeza ibada, kufunga, kutenda mema na kuendelea kuwalea watoto na vijana katika misingi ya maadili, uadilifu, huruma na kumcha Mwenyezi Mungu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here