Rais Dkt.Samia afanya uhamisho na uteuzi wa viongozi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho na uteuzi wa viongozi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uhamisho na uteuzi huo ni kama ifuatavyo:

(i) Dkt. Seif Abdallah Shekalaghe amehamishwa kutoka Wizara ya Afya kwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria.

Dkt. Shekalaghe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. John Anthony Jingu ambaye aliteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania;

(ii) Dkt. Grace Elias Magembe ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya. Dkt. Magembe alikuwa Mganga Mkuu wa Serikali;

(iii) Bw. Charles Ngeleja Kadonya ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki.

Bw. Kadonya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Stephen Patrick Mbundi ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwezi Machi 2026; na

(iv) Prof. Verdiana Grace Masanja ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI).

Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo,tarehe ya uapisho wa Makatibu Wakuu wateule itatangazwa baadaye.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here