Rais Dkt.Samia,Dangote wajadili fursa za uwekezaji nchini

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Dangote Group, Alhaj Aliko Dangote, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Dangote, ambaye ni mwekezaji na mfanyabiashara kinara barani Afrika, ameeleza utayari wa kampuni yake kupanua ushirikiano wa uwekezaji na Serikali katika sekta mbalimbali za kimkakati.

Mazungumzo hayo yamegusa maeneo ya miundombinu ya usafirishaji, uzalishaji wa mbolea nchini na nishati, kama sehemu ya fursa za uwekezaji zinazoweza kuchochea shughuli za kiuchumi nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Dangote amesema,Tanzania ina mazingira mazuri ya uwekezaji na fursa kubwa za kukuza viwanda vinavyoongeza thamani ya malighafi na kuchochea biashara ya kikanda.

"Tumetambua maeneo yenye manufaa makubwa kwa Tanzania na tuko tayari kushirikiana na Serikali kuyaendeleza kwa manufaa ya pande zote,"amesema Dangote.

Kwa upande wake, Rais Dkt. Samia amesema Serikali imepokea na hiyo na kuzielekeza wizara na taasisi husika kuendelea na majadiliano ya kitaalamu kuhusu maeneo yaliyojadiliwa, kwa kuzingatia sera, sheria na vipaumbele vya maendeleo ya nchi.
Amesema,Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kuvutia uwekezaji wenye tija unaochochea ukuaji wa uchumi, maendeleo ya viwanda, uhamishaji wa teknolojia na ajira kwa Watanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here