Waziri wa Fedha afanya mazungumzo na uongozi wa Standard Chartered Bank

DAR-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered anayemaliza muda wake,Bw.Herman Kasekende pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa benki hiyo, Bw.Geoffrey Mchangila katika ofisi ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, Mhe.Balozi Omar amemshukuru Bw.Kasekende kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha sekta ya benki nchini na kuunga mkono utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya maendeleo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha,amempongeza Bw.Mchangila kwa kuteuliwa kuongoza benki hiyo,akiahidi ushirikiano wa Serikali katika kuendeleza ukuaji wa sekta ya fedha na benki, kwa manufaa ya uchumi wa Taifa na maendeleo ya Watanzania kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here