Acheni malezi ya kudekeza watoto,ni chanzo cha mmomonyoko wa maadili

MWANZA-Wazazi na walezi Jata ya Igoma jijini Mwanza wametakiwa kuwa makini na mienendo ya watoto wao na kuachana na malezi dekezi ambayo yamekuwa chanzo kikubwa cha mmomonyoko wa maadili katika jamii.
Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Polisi Kata ya Igoma, Mkaguzi wa Polisi Richard Magoma alipokuwa akizungumza na wakazi wa Mtaa wa Kilimo A uliopo Wilayani Nyamagana, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya Jeshi la Polisi kuishirikisha jamii katika kuzuia na kutanzua uhalifu.

​Mkaguzi Magoma amewakumbusha wazazi hao kuwa malezi ya mtoto ndiyo yanayoamua mustakabali wa maisha yake ya baadaye akisema, "jamii lazima itambue kuwa mtoto umleavyo ndivyo akuavyo."

​Katika mkutano huo, mkaguzi huyo amewasihi wazazi kutoishia nyumbani tu, bali wafuatilie kwa karibu mahudhurio ya watoto wao shuleni na kujenga utaratibu wa kuwasiliana mara kwa mara na walimu ili kujua maendeleo yao.

​Pamoja na masuala ya malezi, Magoma amewataka wananchi hao kutoacha kushirikiana na Jeshi la Polisi, akisisitiza umuhimu wa kutoa taarifa sahihi za uhalifu na wahalifu ili kuufanya mtaa huo kuwa mahali salama pa kuishi.

​Nao baadhi ya wakazi wa mtaa huo wamelishukuru Jeshi la Polisi kwa elimu hiyo wanayoipata mara kwa mara, wakieleza kuwa inazidi kuwapa nguvu na mbinu mpya za kupambana na uhalifu kupitia mpango wa ulinzi shirikishi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here