RUVUMA-Polisi Kata ya Tingi Mkaguzi wa Polisi (INSP) Juma Mbwana akishirikiana na mafundi pamoja na waumini wa Kanisa la Jumuiya ya Katoliki Tingi (AGOSTINO TINGI MISSION) katika ujenzi wa jengo jipya la Kanisa hilo linalojengwa katika Kijiji cha Tingi kilichopo kata ya Tingi Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.

Akiendelea na shughuli hiyo ya ujenzi Julai 28,2026 Mkaguzi huyo amewataka mafundi na waumini hao kuwa mabalozi wa kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia katika jamii pamoja na uhalifu mwingine kwa kuwaelimisha waumini wengine na jamii kiujumla kuhusiana na madhara ya vitendo hivyo katika jamii, huku akiwasisitiza kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu mapema kwa Jeshi la Polisi ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wakati.
Sanjari na hilo pia amewapongeza mafundi kwa hatua waliyoifikia katika ujenzi na kuwaasa kuendelea kufanya kazi hiyo kwa uaminifu na kasi ili jengo hilo liweze kukamilika kwa wakati ili kuanza kutoa huduma ya kiroho kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.


