NJOMBE-Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe amekutana Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mahamoud Hassan Banga Julai 9,2026 amekutana na Chama Cha Madalali Mkoa wa Njombe kujadiliana masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama mkoani humo.
Kamanda amewataka madalali hao kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe katika kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu kwa kutoa taarifa sehemu husika ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao.Pia, amewataka madalali hao kuwa wamoja kwa kushirikiana wao kwa wao kuwafichua wahalifu ambao wamekuwa wakija mkoa wa Njombe kufanya uhalifu kama vile wizi wa viazi na kukimbilia sehemu nyingine.
Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja huo, Mathias Lufunyo amemhakikishia kamanda kuwa wataendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu ili mkoa wa Njombe uendelee kuwa salama.