Magazeti leo Julai 17,2026

Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Kigoma, imeifuta rasmi kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na wapiga kura wanne wa Jimbo la Kigoma Mjini kupinga ushindi wa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi,Clayton Chipando maarufu kama Baba Levo.
Uamuzi huo umetolewa Julai 15, 2026 na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma, Victoria Nongwa ambaye alisema waleta maombi wameshindwa kuithibitishia mahakama madai yao kwa kiwango kinachotakiwa kisheria, hivyo wajibu maombi wote akiwemo Baba Levo na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) hawana kesi ya kujibu.

Jaji Nongwa alisema kuwa hoja zilizowasilishwa na walalamikaji zikiwemo madai ya rushwa, utekaji, kauli zinazodaiwa kuchochea udini na ukiukwaji mwingine wa sheria za uchaguzi hazikuungwa mkono na ushahidi wenye mashiko wa kuishawishi mahakama kutengua matokeo hayo.

Kutokana na dosari za kisheria zilizobainika katika ushahidi wa waleta maombi, mahakama iliamua kulitupilia mbali shauri hilo, hivyo kumfanya Baba Levo kutambuliwa kuwa Mbunge halali wa jimbo la Kigoma Mjini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here